Hosea 10:5-8


5 aWatu wanaoishi Samaria huogopa
kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni.
Beth-Aveni maana yake Nyumba ya Ubatili (au Uovu), jina lingine la Betheli kwa dhihaka.

Watu wake wataiombolezea,
vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,
wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,
kwa sababu itaondolewa kutoka kwao
kwenda uhamishoni.

6 cItachukuliwa kwenda Ashuru
kama ushuru kwa mfalme mkuu.
Efraimu atafedheheshwa;
Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti.

7 dSamaria na mfalme wake wataelea
kama kijiti juu ya uso wa maji.

8 eMahali pa kuabudia sanamu pa uovu
Yaani Aveni kwa Kiebrania, kumaanisha Beth-Aveni , jina lingine la Betheli kwa dhihaka.
pataharibiwa:
ndiyo dhambi ya Israeli.
Miiba na mibaruti itaota
na kufunika madhabahu zao.
Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!”
na vilima, “Tuangukieni!”

Copyright information for SwhKC